Harmonize kuondoka WCB na hali halisi!
0
August 30, 2019
Imekuja kama maajabu vile na mahesabu hayakukaa sawa, ambaye hakurajiwa au hakufikiriwa kuondoka WCB, Harmonize. Imeshangaza wadau wa muziki kidogo kutokana na kujulikana kama mtoto mpendwa wa bosi wa lebo, Diamond Platinumz kutokana na ukweli kwamba Harmonize ndiye msanii wa kwanza kusajiliwa WCB na kufananishwa na Diamond kwa muonekano, aina ya maisha (lifestyle) na mpaka uandishi.
Harmonize aliyeanza gemu toka 2011 lakini akaja kupata kusikika mwaka 2015 baada ya kusajiliwa WCB kwa ngoma yake ya Aiyola na baadae Bado ya mwaka 2016 aliyomshirikisha Diamond, hakuonekana angeondoka baada ya msanii mwenzie Rich Mavoko aliyejitoa kutokana na vinasaba vinavyolandana na bosi wake, Diamond.
https://www.hillywood.rw/wp-content/uploads/2019/02/harmonize_ft_diamond_bado-video.png
Diamond na Harmonize kwenye uchukuaji wa video ya Bado, 2015
Kuondoka kwa Harmonize ni mchakato ambao una majibu chanya kwake kwa upande mkubwa na sanaa yake kijumla, kwakuwa ameshajenga jenga jina lake kiasi kikubwa kwa uwepo wa lebo ya WCB na sasa ya kwake ya Konde Gang. Mafanikio ya kutoa EP yake hivi karibuni ya Afro-Bongo iliyokuwa na ngoma 4, msanii anayewania tuzo za AFRIMMA na akiwa na tuzo kadhaa kwenye kabati lake kama vile Video bora kwa chipukizi ya WatsUp TV, Mwimbaji chipukizi wa African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) na mwimbaji chipukizi kwenye African Entertainment Awards (AEAUSA) na nyinginezo. Angalia lebo, menejimenti , mashabiki wengi (fan base) na brand aliyoko nayo, si msanii wa kubeza!
Image result for harmonize afrimma 2019
Mojawapo ya tuzo ambayo Harmonize anawania
Huyu Rajab Abdul Kahali maarufu Harmonize, mzaliwa wa Chitoholi, Mtwara tayari amejitoa na ana sababu zake na ki ukweli hawezi kukaa tena pale ikiwa lengo lilikuwa kushikwa mkono. Mtoto akikua anaondoka ntumbani na yeye anaenda kuanziasha mji wake, baba ana sheria za nyumba yake si wote hufurahia kama mtoto ukiwa mkubwa uhuru ukiupata kuna vitu utaona baba anakubana. Vyema, anzisha mji wako.
Image result for q chilla na harmonize
Harmonize na Q Chillah
Harmonize ameweza kumsimama tu mkongwe Q Chilla akatoa The Return EP ni jambo kubwa na heshima kubwa aliyoifanya, katengeneza mizizi tayari. Moja ya maeneo ambayo yatamletea changamoto kama kulikuwa hakuna maafikiano mazuri kutokana na figisu za chinichini za WCB;
Uwepo wa kampuni yake na Diamond ya video Zoom Production chini ya Director Kenny ambayo ukiangalia imefanya video kali, kama vile Inama ya Diamond na Fally Ipupa, Tetema ya Ravanny na nyinginezo. Hapa kuna nini? Kama mambo hayatokaa sawa kuna uwezekano biashara ikawa ngumu kwa wao kuwa partners na mwenzake. Kama hajaondoka vizuri, ktakuwa na changamoto hapa.
http://inyarwanda.com/app/webroot/img/201908/images/harmonize0-3594231566983888.jpg
Diamond (kulia) na Harmonize
Ushawishi, ukongwe na uwezo wa mameneja wanaosimamia muziki wa WCB, Sallam SK, Mkubwa Fella na Babu Tale ambao wana mnyororo mrefu wa kufahamika na ukongwe kwenye kazi hii ya muziki kwa muda mrefu. Tale alianza na wasanii kama Tip Top, Fella akiwa na TMK Wanaume Family na baadae Yamoto Band, wote tangu miaka ya 2000. Sallam SK alikuwa muandaaji wa shoo za muziki hapa nyumbani hata kwa wasaniii wa kimataifa akiwa kwenye klabu maarufu ya Element, yeye ndiye alimuunganisha Diamond na Davido mwaka ndiyo wakafanya nyimbo ya My Number One Remix na Diamond kuamua kufanya nae kazi moja kwa moja.
Image result for sallam, babu tale na mkubwa
Mameneja wa WCB, Babu Tale(katikati), Sallam SK (kulia) na Mkubwa Fela
Mameneja hawa wana ushawishi mpaka kwa viongozi wakubwa wa nchi akiwemo Rais mstaafu wa Dr. Jakaya Kikwete na wengineo. Kwa hili Harmonize kama hakukaa nao vizuri kuna changamoto itatokea kwenye muziki wake.
Kupungukiwa kwa mashabiki ambao ni WCB damu hii ni kutokana na muziki wa Tanzania kuwa na makundi mawili makubwa, upande wa Diamond na WCB na kule kwa AliKiba na RockStar. Ushindani huu umekuwa mzuri kibiashara lakini ukiangalia figisu za WCB kibiashara ni kubwa sana katika muziki lakini mashabiki wanapenda kugawanyika kwa haraka-haraka mitandaoni wameonesha kutomfuata (unfollow) Instagram na pengine kwenye tuzo zinazoendelea kushindwa kumpigia kura na uizingatia WCB ni familia imejengwa na mashabiki wa Diamond, Harmonize, Rayvanny na wasanii wote wanaounda WCB.
Image result for wcb wasanii
Wasanii wanaounda WCB, wapili na watatu kutoka kulia, Harmonize na Rich Mavoko wamekwishajitoa
Kwa upande huu kuna upepo unashuka kidogo kwa Harmonize, kwa hili likiendelea linaweza kuwa changamoto kwake, lakini haimaanishi atashindwa. Anaweza na namkubali kinoma Inabana aliyoshirikiana na Mganda Eddy Kenzo iko vizuri sana na inaonyesha itafanya vizuri. Let wait him shining!
Kumbuka hapohapo, Rich Mavoko alipoteza channel ya Youtube ambayo iliweka chini ya kampuni na ilikuwa na subscribers zaidi ya milioni moja, akaanza upya. Huoni hii ni changamoto kwenye biashara kama naye mkataba wake alisaini chini ya kampuni? Tazama akaunti yake yenye subscriber milioni moja na laki moja na zaidi mpaka sasa, na wimbo wake wa Kwangaru uliofikisha watazamaji zaidi milioni 50, na tayari ana plaque ya Youtube. Japo mpaka sasa wimbo aliyoshirikiana na Eddy Kenzo ameweka kwenye Youtube yake. Wacha tuone!
Unadhani akizipoteza kama Rich Mavoko, atakuwa amepoteza kiasi gani cha pesa kwa utazamaji wa Youtube? Na ukizingatia hilo, Harmonize ni miongoni mwa wasanii wa Afrika, akiwemo Diamond wenye subscribers zaidi ya milioni moja!
Hayo ni machache kama kwa Harmonize kuamua kujitoa WCB kutokana na hali halisi ya muziki wetu ulivyo na mazingira ya Wasafi. Ila tayari ana uwezo na hizi ni changamoto ndogondogo ambazo akiamua anaweza kuzipotezea, akaongeza juhudi akafanya vizuri zaidi hasa kimataifa. Kikubwa asisikilize mashabiki mitandaoni inaweza kumpa msongo wa mawazo kwasababu wasanii wengin wamepitia hii hali!
Tags