Harufu kali ya ushuzi yasimamisha Bunge kwa muda

Mjadala  mkali juu ya hali ya masoko ulikatizwa ghafla kwa harufu kali ya ushuzi.

Kadhia hiyo haikutokea sokoni au mtaani, bali ni kwenye ukumbi wa Bunge la Kaunti ya Homa Bay, Magharibi kwa Kenya.

“Mheshimiwa Spika, mmoja wetu hapa amechafua hali ya hewa,” alisema Julius Gaya kwenye kikao cha Bunge.

Lakini mjumbe aliyerushiwa lawama za kujamba alikanusha vikali akisema: “Sio mimi. Siwezi fanya kitendo kama hicho mbele ya wenzangu.”

Katika jitihada za kupambana na harufu hiyo, Spika Edwin Kakach akaamuru wajumbe wote watoke nje kwa muda.

Ripoti pia zinaeleza kuwa aliagiza marashi ili kuleta harufu nzuri. “Lete (marashi) ya aina yeyote utakayoyakuta ofisini kwangu, hatuwezi kuendelea kukaa kwenye mazingira ya kunuka.”

Hata hivyo inadaiwa harufu hiyo ilikatika kabla ya marashi hayo kupatikana hali iliyoruhusu kikao kuendelea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad