Hi Hapa Ratiba Nzima ya Simba kuelekea Simba day,


Maadhimisho ya Simba week yalianza rasmi tarehe 31/7/2019 ambayo pia ndio siku akikosi cha klabu hiyo kimewasili nchini kikitokea Afrika ya Kusini sehemu ambako kilienda kwa ajili ya maandalizi ya ligi pamoja na michuano mingine mikubwa katika bara la Afrika hasa michuano ya klabu binghwa barani Afrika.



Tarehe 31-7-2019:- Kusaini mkataba wa miaka miwili na kampuni ya kutengeneza vifaa ya UHL ambayo inatengeneza jezi na vifaa vya mazoezi.
Tarehe 1-8-2019 kutambulisha jezi mpya kwa msimu 2019/2020 majira ya saa 6 kamili usiku ikiwa ni ya nyumbani, ugenini, na ya ziada ambazo zitatambulishwa rasmi kupitia mitandao wa kijamii ya Simba.


.Uuzaji wa jezi nchini nzima ambako klabu itatangaza wapi jezi hizi zitapatikana pamoja na bei ya jezi hizi ingawa suala la bei tayari limeshajulikana ambapo bei ya jezi moja ni shilingi za Kitanzania 30000/=

.Kutakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzindua kadi mpya ya benki (Smart Card) za wanachana na mshabiki wa Simba.

.Kuanza uuzaji wa tiketi za Platnum na Platnum plus kwa ajili ya mtanange kati ya Simba na klabu ya Dynamos

3.Tarehe 3-8-2019 Kampuni ya Sportpesa kwa kushirikiana na klabu watawatembelea na kuwatia moyo watoto waishio katika magumu.



. Wachezaji wa Simba kwenda kutoa misaada katika Hospitali ya Ocean Road Jijini Dar Es Salaam, lakini pia ombi limetolewa kwa wanachama na mashabiki wote wa Simba nchini nzima kuungana na klabu popote pale nchini kwenda kutembea Hospitali yeyote iliyokaribu yako kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali kwa watu waishio katika mazingira magumu.

. Kuchangia damu

. Kuzindua wimbo maalumu wa Simba. Nia ya kufanya hivi ni kuongeza hamasa kwa wanachama wa Simba na mashabiki wote wa klabu ya Simba.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad