Mhe.Ikupa amesema hayo jijini Dodoma wakati akifunga kikao cha Baraza kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania [UWT]Kwa mkoa wa Dodoma.
Ikupa ametaja Nyanja mbalimbali ambazo Serikali ya awamu ya Tano imetekeleza ikiwa ni pamoja na kupambana na Dawa za kulevya ambazo zilikuwa zikipoteza vijana na kurudisha nyuma uchumi wa nchi,Uimarishaji wa Miundombinu ikiwa ni pamoja na Umeme,Barabara,Reli,Afya,Elimu bure na Usafiri wa anga pamoja na uwezeshaji wa Mikopo kwa makundi maalum ikiwa ni pamoja na vijana,wanawake na watu wenye ulemavu.
Hata hivyo ,Naibu Waziri huyo amechangia Jumla ya mabati 10 yenye thamani ya Tsh.360,000 Kwa UWT Dodoma kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Elimu huku jumla ya Tsh.milioni moja ,laki nane na hamsini elfu zikichangiwa kwenye harambee ya baraza hilo.
Kwa upande wao Mjumbe wa Kamati kuu Hadija Shalo [Keisha] na mjumbe wa Baraza kuu Taifa UWT,Chiku Mugo amempongeza Rais Magufuli pamoja Naibu Waziri Ikupa Kwa Mchango huo huku wakiwapongeza wadau wengine kwa kuendelea kuiunga UWT Katika kufanikisha miradi mbalimbali ya Maendeleo
INNALLILAHI WAINNA ILAHI RAAJIUNN.
ReplyDelete