India imechapisha orodha ya mwisho ya watu milioni 1.9 iliyowavua uraia wake Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.
Sajili ya kitaifa ya raia(NRC)ni orodha ya watu ambao wanaweza kuthibitisha kuwa waliinga nchini humo kufikia mwezi 24 Machi mwaka 1971, kabla ya Bangladesh kupata uhuru wake kutoka kwa Pakistan.
Watu ambao hawajajumuishwa katika sajili hiyo wana siku 120 kukata rufaa dhidi ya hatua ya kuvuliwa uraia wa nchi hiyo.
Haijabainika nini kitakachofuata baada ya hatua hiyo kutekelezwa.
India inasema mpango huo ni muhimu katika mchakato wa kuwabaini wahamiaji haramu kutoka Bangladesh.
NRC ilibuniwa mwaka 1951 kutofautisha mzaliwa wa Assam ambaye ni raia halisi na mhamiaji kutoka taifa jirani la Bangladesh.
Tayari maelfu ya watuwaliokamatwa wanazuiliwa katika kambi ya muda kwa kushukiwa kuwa raia wa kigeni, lakini kuna hofu ikiwa watakubalika walikotoka.
Mpango huo umezua gumzo kali baadhi ya watu wakidai ni"hujuma" dhidi ya jamii ya Assam walio wachache.
Rasimu ya sajili hiyo iliyochapishwa mwaka jana iliwatenga watu milioni nne.
Sajili ya Kitaifa ya raia ni nini?
Sajili ya NRC ilibuniwa mwaka 1951 to kutofautisha mzaliwa wa Assam ambaye ni raia halisi na mhamiaji kutoka taifa jirani la Bangladesh.
Sajili hiyo imefanyiwa mabadiliko kwa mara ya kwanza.