Jeshi la Polisi Latoa ONYO Kwa Madereva Nchini


Jeshi la Polisi nchini limetoa ufafanuzi na kuweka msisitizo kwenye katazo alilotoa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam tarehe 05/08/2019 kuhusu kupiga marufuku magari kufunga taa za vimulimuli au za rangi rangi, taa zenye mwanga mkali (spot light) na kufunga ving’ora kwenye magari ya kiraia au watu binafsi na pikipiki za kiraia.

Akitoa tamkoa hilo Msemaji wa Jeshi hilo SACP, David Misime amesema kuwa, katazo hilo ni kwa nchi nzima, kutokana na kujitokeza kwa baadhi ya watu walioamua kufunga vimulimuli na ving’ora na kuvitumia wawapo barabarani na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara.

Wamefunga vifaa hivyo kutaka kupewa kipaumbele wawapo barabarani kwa kujua au kwa kutofahamu kuwa ni kinyume na sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

Na kwa mujibu wa sheria ya usalama barabarani sura ya 168 ya mwaka 1973 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002 kifungu cha 39 B (I) na (2) kinafafanua juu ya matumizi ya ishara ikiwepo ving’ora na vimulimuli.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad