'Jezi mpya za Simba SC zawatibua Wazee'



Mzee wa klabu ya Simba Chahal Chahali amesema kuwa jezi zilizozinduliwa jana kwa ajili ya matumizi ya msimu huu kuwa si rangi za klabu hiyo maana wao wana rangi mbili nyekundu na nyeupe.

Hapo jana Kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya UHL Sport Dubai litangazwa kushinda tenda ya kutengeneza jezi za klabu ya Simba SC kwa ajili ya msimu wa 2019/2020 ambapo klabu hiyo imeingia rasmi mkataba wa miaka miwili na kampuni hiyo.

"Simba inavaa jezi ya njano kweli?, hayo mambo yametoka wapi. Rangi ya yetu ni nyekundu na nyeupe, leo zimetoka jezi hizi mpya za rangi ya njano, hizo na nyeusi wanavaa Yanga," amesema Mzee Chahal akiwa na Mzee Kilomoni.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad