Jinsi Ya Kujua IMEI Ya Simu Yako Iliyoibiwa na Namna ya Kuifunga Simu Isitumike Tena
0
August 12, 2019
IMEI kwa kirefu chake ni ‘International Mobile Equipment Identity‘ ambapo kwa haraka haraka ni namba ambazo zinakuwa kama utambulisho wa kifaa na katika simu, mara nyingi zinakuwa na tarakimu15. Namba hizi huwa hazifanani na zinakuwa katika kifaa kimoja tu.
Faida yake inakuja pale unapokuwa umepoteza kifaa chako kwa sababu namba hiyo ni moja tu kwa kifaa kile hivyo itakuwezesha kuweza kufuatilia nyendo za simu hiyo kama ikiwa imeunganishwa na intaneti.
Mbali na kukusaidia kuipata simu hiyo, vilevile, unaweza ukaamua kufuta kila kitu na kuifunga kabisa simu hiyo kutoweza tumika tena kupitia IMEI ya simu hiyo.
Jinsi ya kuangalia IMEI namba ya simu yako
Andika *#06# kisha bonyeza kitufe cha kupiga
Baada ya hapo simu yako itakuletea IMEI namba ambapo kama simu yako au kifaa chako kina laini mbili basi kutakuwa na IMEI namba mbili
Namba hii pia unaweza kuipata katika boksi la simu ama nyuma ya simu hiyo baada ya kutoa betri, utaijua kwa kuwa huwa ni tarakimu 15.
Nakili namba hizo pembeni. Itakusaidia sana siku ukipoteza au kuibiwa simu yako
===>>Hayo yote yanawezekana kama ukiwa na simu yako. Vipi sasa ikiwa simu yako umeipoteza au imeibiwa? utafanyaje?
Jinsi ya Kupata IMEI Ya Simu yako iliyoibiwa au uliyoipoteza
Kama huna simu yako karibu kwa maana kwamba imeibiwa, unaweza ukapata IMEI kwa kutumia Find my device kwa wale wa Android na Find My Phone kwa wale wanaotumia Apple.
Kujua IMEI kwenye simu ya Android
Kwa watumiaji wa Android , unaweza kupata IMEI yako kwa kutumia akaunti ya Google uliyokuwa unatumia katika PlayStore.
==>>Fanya yafuatayo:
Ingia katika Android Device Manager kupitia kompyuta
Ingia kupitia akaunti yako ya Google ambayo ulikua unaitumia katika simu yako.
Ukifanikiwa kuingia humo utaona vifaa vyote ambavyo vimeungwa na akaunti hiyo, unaweza chagua kifaa husika na kuone taarifa zake ikiwemo IMEI.
Kujua IMEI kwenye iPhone
Kwa kutumia kompyuta yako ingia katika tovuti ya Apple
Ingia katika Akaunti yako kwa kutumia Apple ID
Ukishaingia nenda katika orodha ya vifaa kisha chagua jina la kifaa
Taarifa za kifaa husika zitatokea ikiwemo na IMEI ya kifaa hicho.
Tags