Jux Aanika Sababu ya Kutemana na Vanessa Mdee


Nyota wa muziki wa miondoko ya R&B hapa Bongo Juma Jux kwa mara ya kwanza amezungumza juu ya nini kilisababisha kutengana kwake na Vanessa Mdee.

Akifanyiwa mahojiano na Mtangazaji wa Clouds FM kupitia chaneli yake ya YouTube ya Dozen Selection, mkali huyo anayetamba kwa sasa na ngoma ya Sumaku amesema kwamba kuvunjika kwa uhusiano wake na Vanessa kwa mara ya kwanza mwaa 2017 ilisababishwa na picha alizopiga Vanessa na mwanamuziki kutoka Nigeria Ice Prince na kuposti Instagram hazikuwa na taswira nzuri, hali iliyomfanya Jux kupata mshtuko. Vanessa na Ice Price walikuwa wakifanya video ya wimbo wao.

Vanessa alikuwa amesafiri na nikawa naangalia picha Instagram, nikaona picha kapiga na Ice Prince, na kuna watu nilikuwa nimekaa nao, wanakaniulza sasa picha gani hizi watu wanapiga. Ile mijazo ile. Hapo kulikuwa kumetokea vile vitu vya kina Trey songz. So nikamtext, what is this, futa. Akaniuliza whats wrong with the picture I’m performing. Ni kamwambia hiyo picha sio poa. So mimi nikawa nime ‘panic’ na ile ikasababisha ugomvi mkubwa. Akawa disappointed sana, alikuwa anafanya kazi. Mambo ya wivu. Sasa katika zile hasira nikamwambia katafute boyfriend mwingine. To be honest nilimuonea sana and it was not right. So kile kitu ndiyo kilikuwa chanzo cha kukosana kwetu. Tukaenda miezi tisa bila kuongea kabisa. Jux amesema.


Jux ameongeza kuwa:

Nilikuwa na vanessa kwa miaka 6. Naweza kusema kuwa mahusiona yangu na Vanessa yamenitengeneza sana kwa njia nyingi kuliko mahusio yeyote yale. Na pia nilipigana sana kutoyapoteza and niliumia sana. Na mpaka kufika hatua ya kuachana tulikuwa tumeona kuwa haiwezekani tena. Na mtu yeyote ambaye atapata nafasi ya kuwa na mahusion na Vanessa Mdee atakuwa mwanaume mwenye bahati sana. She is a very beautiful and smart woman.

Kwa bahati nzuri, aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds FM Marehemu Ruge Mutahaba aliingilia kati na wawili hao waliweza kurudiana tena.


Jux na Mpenzi wake mpya Nayika
Hata hivyo, mwaka huu wa 2019 uhusiano wao umeingia tena dosari na kuamua kufikia hatua ya kuachana kabisa na kila mtu aendelee na mipango yake mingine.

Hivi sasa Jux yuko katika penzi zito na msichana kutoka Thailanda Thailand. Kwa upande wake Vanessa bada hajabainisha mpenzi wake mpya.

Unajua mimi nikiwa kwenye mahusiano napenda sana kuonesha mpenzi wangu. Sio eti nataka kumuumiza Vanessa bali hivyo ndiyo mimi napenda. Juma Jux.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad