Kabendera Apandishwa Kizimbani, Hakimu Apata Udhuru

Kabendera apandishwa kizimbani, Hakimu apata udhuru
Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwandishi wa habari za uchunguzi Erick kabendera imeahirishwa hadi Septemba 12 mwaka huu itakapotajwa tena.

Kesi hiyo imetajwa mbele ya Hakimu Janeth Mtega baada ya Hakimu Rwizile kupata dharura na kutoweza kufika mahakamani.

Aidha upande wa serikali umedai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba wapewe muda zaidi ili kukamilisha upelelezi.

Hata hivyo Wakili wa utetezi kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania( THRDC), Jebra kambole, ameomba mapendekezo mawili, upande wa serikali kuongeza nguvu Katika upelelezi Kwani mshtakiwa hadi sasa hana dhamana.

Kabendera anashitakiwa kwa Makosa matatu ya Kujihusisha na genge la uhalifu, kukwepa kulipa kodi na utakatishaji fedha
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad