Kaka yake Lissu afunguka, ‘Hii kesi sio ya hovyo’

Kaka wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Singida Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, Alute Mughwai amesema kuwa kesi ya maombi iliyofunguliwa na Lissu sio ya hovyo kama inavyozungumziwa na upande wa serikali.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam mara baada ya majibizano makali ya kisheria kutokea mahakamani, ambapo upande wa serikali ulipeleka mawakili 15 kwa ajili ya kuweka pingamizi dhidi ya kesi ya Tundu Lissu.

Amesema kuwa kesi hiyo ina umuhimu mkubwa ndiyo maana upande wa serikali umepeleka mawakili 15 ikiwa ni pamoja na mwanasheria mkuu, hivyo kuonyesha kuwa kesi hiyo ina umuhimu wa kipekee kwa mustakabali wa nchi.

”Tunataka mahakama itueleze kama ni sahihi kwa mbunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushambuliwa mchana kweupe, halafu hapewi huduma ya matibabu, baada ya hapo anaondolewa ubunge, kwa hoja kwamba hayupo bungeni na hawajui alipo,”amesema Mughwai

Hata hivyo, maombi hayo ya Lissu ambayo yalitakiwa kuanza kusikilizwa hapo jana mbele ya Jaji Sirilius Matupa, hayakusikilizwa baada ya upande wa serikali kuwasilisha pingamizi la awali lenye hoja tisa kutaka shtaka hilo lifutiliwe mbali.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Alute, Je na wewe ni mpotoshajiau ni mhemuko.

    Kwanza kutumia neno KESI kwa uhalisia ni Hati ya Maombi ya Dharura. hii inadhihirisha uelewa wako mfinyu wa sheria.Na unaelewa fika asilimia 98 ya hati za namna hufungwa na kutupiliwa mbali.

    Jamuhuri wao sawa na wewe ningekuomba ukajifunze kwa adv.. Manyanya au prof Msafiri au M.Ismail AG (mstaafu) au Adv.Albert Msando.

    Jua mshahara Hewa toka kwa walipa kodi masikini ni haramu kuliwa na msaliti aliye ona fahari kuipaka Matope nchi yetu na kujijengea mazingira ya ki Ukimbizi ( asylum SEEKER) huko Ulaya na Maleekani (Alute, Unajua file lake kafungulia wapi )

    Na kama una lengo la kutafuta Kiki na kupotosha , basi hapa mmekosea kama alivyo sema Fatma siku ile.kwamba mashiohaina na mkasema tutajaribu.

    Tafadhali sitisha upotoshaji na matumizi ya lugha sahihi yanayo enda sambamba na uhalisia.

    Msomaji wa kawaida anaweza kuelewa ndivyo sivyo.

    ReplyDelete
  2. Eheee...!!

    Nyie kweli mnachezea Mahakama.
    UNATAKA MAHAKAMA IKUELEZE KAMA NI SAHIHI MBUNGE KUSHAMBULIWA MCHANA..?????

    KWELI HAMNA MASHIKO.

    HAYA MIE MBU MBU MBU MUNGU WA RELI NASE BORA INGEKUWA GIZANI BAAYA YA KUSHIBA KABLA YA KULALA NA KAMA PANADOLI IPO BASI BOLA KWANZA ANGEPATA TEMBE MBILI NA MAJI YA VUGU VUGU MULAINISHA TUMBO NA MCHANGO ILI AWEZE KUENDESHA.

    HIVYO MNADHANI MAHAKAMA ZERU ZINA WAKATI WA KUPOTEZA NA KUZIDHIHAKI..??? TUNA MENGI YA KUFANYA NA KUTATUA YA MSOLWA BUTIMBA NA IRINGA NA ISANGA.MKTAKA CHA NDIMU MNAKARIBISHWA UWANJA WA BARAFU.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad