Wanasiasa pamoja na wadau wengine akiwemo aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu wameendesha kampeni maalumu ijulikanayo kama jiondoe Vodacom kwa kitendo cha kuvujisha mawasiliano ya wateja wao.
Kampeni hiyo ambayo wameitangaza katika mitandao ya kijamii ikiwa imelenga kuwepo na udhibiti wa mawasilino ya mteja bila kutolewa kwa taarifa zake.
Lissu kupitia akaunti yake ya Twitter amesema anasusia huduma za mtandao wa Vodacom na rasmi anaachana nao.
“Nimesusia huduma za mtandao wa Vodacom Tanzania na rasmi anaachana nao,” aliandika Lissu.
Nimesusia huduma za mtandao wa @VodacomTanzania na rasmi naachana nao. #JiondoeVodacom #FreeErickKabendera— Tundu Lissu (@tundu_lissu) July 31, 2019
#FreeErickKabendera !! #JiondoeVodacom ! Nimekuwa Mteja wa VODACOM kwa MIAKA zaidi miaka 10!! Najua nitaathirika kimawasiliano pale nitakapo SITISHA matumizi ya NAMBA yangu!! Lakini kwa HAYA yanayoendelea, NIKO TAYARI KUJIONDOA VODACOM!!!Tususie BIDHAA za WAKANDAMIZAJI!!!— Halima James Mdee (@halimamdee) July 31, 2019
#FreeErickKabendera Mkakati huu wa kususa kununua,kuuza,huduma za Makampuni/Biashara zinazo haribu haki/demokrasia utafanikiwa sana,nasisitiza tuwe WATII tu,hatuitaji kuwa barabarani tunahitaji UTII wa kuitika wito utakao kuwa una tolewa.Mimi NITAKUWA MTII— Godbless E.J. Lema (@godbless_lema) July 31, 2019