Kampuni ya Green Mile Safari imeeleza kuwa taarifa zinazosambaa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla ameifutia umiliki wa kitalu hicho cha kitalii si za kweli.
Imesema inazitafsiri taarifa hizo kama mwendelezo wa mkakati wa kuichafua kampuni hiyo na kuiharibia biashara kwani haina taarifa yoyote kutoka Serikalini kuhusu kufutiwa umiliki
Aidha, imeongeza kuwa shughuli za uwindaji wa kitalii za kampuni hiyo zitaendelea kama kawaida kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni za nchi
Hata hivyo, Waziri Kigwangalla kupitia mtandao wa Twitter ameshangaa taarifa hiyo na kusema “Mtu anakanusha utafikiri anajipa yeye hicho kitalu. Waziri mwenye mamlaka ya kugawa vitalu amefuta umiliki wake, anabisha vipi sasa? Mwenye kitalu kachukua, wewe unakataa! I thin”
Hapo jana, Waziri wa Utalii na Maliasili, Dk. Hamisi Kigwangalla alifuta umiliki wa kitalu cha uwindaji cha kitalii cha Lake Natron (East) kilichokuwa kinamilikiwa na kampuni ya Green Miles kuanzia leo Agosti 7, 2019.