Katibu wa CCM Karatu amwangukia Magufuli ,ufisadi kiwanda cha maziwa
0
August 11, 2019
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Katibu wa Ccm wilaya ya Karatu Shaban Mrisho amemuomba Raisi Magufuli kuwachukulia hatua waliofanya ufisadi na kukifilisi kiwanda cha maziwa cha Ayalabe kwani kwa kufanya hivyo wanahujumu juhudi za kufukia uchumi wa viwanda na uchumi wa kati.
Akizungumza wakati kamati ya siasa ya Wilaya ikitembelea kiwanda hicho na kuijionea mashine za kisasa za gharama kubwa zikiwa zimekaa kwa muda wa miaka mitano bila kufanya kazi baada ya kiwanda hicho kusimama kwa kufilisika.
Mrisho amemuomba Magufuli kuingilia kati mara baada ya kuona watuhumiwa wa ufisadi wa kiwanda hicho kesi zikipigwa dana dana huku wengine wakiwa huru mitaani .
Naye Katibu Mwenezi wa Wilaya hiyo Danstan Panga amesema kuwa hatua kali zinapaswa kuchukuliwa na kuhakikisha kuwa wale wote wanaodaiwa na kiwanda hicho na walichota fedha kwa njia ya kifisadi kiuhakikisha kuwa wanazirejesha.
Mkuu wa Wilaya hiyo Theresia Mahongo amesema kuwa tayari alishafanya juhudi za kuunda tume ambayo ilibaini ubadhirifu huo na kupendekeza hatua za kuchukua ili kunusuru kiwanda hicho kisife.
Tags