Kauli 12 Alizozitoa Waziri Mkuu Majaliwa Wakati wa Tukio la Kuwatambua Waliofariki kwa Moto Morogoro


1.Niko mbele yenu kumwakilisha Rais  Magufuli kuungana nanyi siku hii ya huzuni kubwa, Rais alipokea taarifa hii jana. Kwa taarifa mpaka sasa waliofariki ni 69, tumepata taarifa tukiwa hapa mwenzetu 1 aliyebebwa kwa Helikopta amekufa njiani.

2.Rais amepata taarifa hizi kwa masikito makubwa, ameendelea kuwaombea marehemu na majeruhi, amewaomba utulivu ndugu, jamaa, na marafiki mlioguswa na tukio hili, kwa uzito wa jambo hili amelitangazia taifa siku 3 za maombelezo kuanzia jana.

3.Yeye anaugeni mkubwa wa Marais 16 wanaoingia nchini kwa maandalizi ya mkutano wa SADC, kwa hiyo mtambue kwamba uzito wa kuwapokea wenzake pamoja na tatizo hili kubwa na kwa kuwa sisi wasaidizi wake tupo akaamua kunileta kwenu.

4.Nimepita hapo hali si nzuri ndugu zetu wameungua sana, na iko hatari wengine tusiwafahamu kabisa, lakini hatutawanyima nafasi kuwatambua ndugu zetu, na kwa kuwa tulikuwa nao tangu jana asubuhi, tutawapa nafasi ya kuwatambua.

5.Kama una mashaka kuna ndugu yako humuoni tangu jana, tumekupa nafasi ya kuja kutoa taarifa, na tutakupima DNA, ili kutambua ndugu yake kwa sababu tumechukua vinasaba vya marehemu wote ili kuwatambua.

6.Nitaunda tume ianze kuchunguza kuanzia leo hadi Ijumaa, ichambue vizuri na hata kama mimi nitakuwa sijawajibika wanitaje, baada ya hapo serikali tutajua cha kufanya.

7.Manispaa kuna kitengo cha Fire, japo najua walikuja kwa kuzima, ila je walikuja baada ya muda gani? tumesisitiza umakini na uwajibikaji, nasikia tumeokoa mafuta sasa tumeokoa yakiwa yameisha? nitaunda tume wanijibu haya maswali madogo.

8.Hata kama mimi nimehusika wanitaje tu, hatuwezi likapita hivi.

9.Ajali za aina hii Tanzania si mara ya kwanza ilitokea Mbeya niwasihi Watanzania ukiona gari limeanguka usilitumie kama fursa, ukawaokee binadamu walio pale.

10. Je huu muda ambao walikutana hawa ndugu zetu waliotangulia mbele za haki kwa ajili kutoa mafuta, ni nani aliwazuia? mimi ninajua Trafiki huwa wanakuwa na haraka sana, ajali inapotokea, nani alihusika kuwazuia.?

11.Vyombo vya habari mnaendelea kuhabarisha watanzania, kwenye vyombo vya habari tuelewane jambo moja kuhusu takwimu, jana zilikuwa zinachanganya msiseme suala la takwimu, anaeyeweza kusema ni Mkuu wa Mkoa.

12.Naogopa msije mkaingia kwenye sheria ya takwimu, kuanzia sasa chukueni za Mkuu wa Mkoa, mlisababisha jana nikazungumza uongo nikiwa na wasomi wa Vyuo Vikuu, nikaona taarifa wako 100 ikaja nyingine 120, na mimi nikataja hiyo idadi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad