Kenya Yatupiga Gapu Kubwa Tanzania...Unaambiwa Wameanza Kuuza Mafuta yanayochimbwa Nchini Humo


Rais Uhuru Kenyatta leo amezindua usafirishaji wa mafuta ghafi yanayochimbwa nchi humo katika Kaunti ya Turkana ambayo yanaenda kuuzwa nje ya nchi

Rais Kenyatta ameshuhudia meli yenye mapipa 200,000 ya mafuta yenye thamani ya Ksh. Bilioni 1.2 (zaidi ya Tsh. Bilioni 26.6) ikiondoka kwenda Uingereza

Kuondoka kwa meli hiyo katika bandari ya Mombasa kunaifanya Kenya kuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki kuuza mafuta ghafi inayoyachimba

Katika hatua hiyo, Kenya imesema inatumia shehena hiyo ya kwanza kujaribu soko la Dunia kabla haijaanza kuuza kwa kiwango kubwa zaidi

Rais Kenyatta amesema "Kuondoka kwa meli hii kunaashiria siku mpya kwa Kenya na mwanzo mpya wa ustawi mkubwa kwa Wakenya wote"

Aidha, amesisitiza kuwa "Tutahakikisha maliasili za Kenya zinatumika kwa ufanisi na katika hali itakayoleta faida kubwa leo lakini bila kuharibu faida kwa kizazi kijacho"

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad