Wakenya Alhamisi, Agosti 15, walipigwa na butwaa baada ya mahabusu waliokuwa wameratibiwa kufikishwa mbele ya jaji wa mahakama ya Kibera kulewa chakari.
Mahabusu hao walifika kwenye mahakama hiyo lakini ikawa ngumu kwa wao kujibu mashtaka kwani wengi walizidiwa na kulala chini kifudifudi.
Wakenya walilalamika kwenye mitandao ni vipi maafisa wa polisi waliamua kuwafikisha walevi mahakama ikizingatiwa hawangeweza kujibu mashtaka yoyote.
Haikubainika ni viti washukiwa hao walipata kuwa walevi kwani kwa kawaida hakuna pombe ambayo hukubaliwa kwenye vituo vya polisi. Vile vile katiba inaruhusu mshukiwa kuzuiliwa kwa masaa kadhaa mradi tu yasipite 24 na hivyo washukiwa hao wangezidi kutuliza kituoni mpaka pombe itulie.
Onyango Ochieng Jr.
But why would you even take a drunk to court!!! These are people who should be granted free bail at the police station and warned not to repeat their drinking. Otherwise, we are wasting courts time. Let's leave Judiciary to handle more serious issues ailing the country .