Kesi ya Benard Membe Dhidi ya Cyprian Musiba Yakwama


Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imekwama kusikiliza kesi ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Benard Membe dhidi ya Cyprian Musiba kwa sababu Jaji hayupo.

Kesi hiyo namba 220 ya mwaka 2018 ilipangwa kusikilizwa leo baada ya pande mbili baina ya mlalamikaji na mlalamikiwa kuwasilisha majibu yao.

Akizungumza na Waandishi wa Habari nje ya Mahakama Wakili wa Membe, Jonathan Mndeme amesema shauri hilo lilipangwa kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

Wakili Mndeme amesema kuwa  shauri hilo limeahirishwa hadi Oktoba 3, 2019 mbele ya Msajili kwa sababu Jaji aliyepaswa kusikiliza shauri hilo hayupo.

Katika Kesi hiyo iliyoitwa kwa mara ya kwanza Februari 26, 2019, Membe amemshtaki Musiba, Mhariri wa gazeti la Tanzanite na wachapishaji wa gazeti hilo ambapo anawadai Sh. Bilioni 10 kwa madai wamemchafua.

Musiba katika kesi hiyo anashtakiwa kwa kumtuhumu Membe kuwa anamhujumu Rais John Magufuli asitekeleze majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo huku akidai kwamba mbinu mojawapo ya kukamilisha hujuma hizo ni maandalizi anayofanya kugombea urais mwaka 2020 kupitia CCM.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kumbe aishawahi kuwa Wazziri wandani.
    Mbona Vioja mahakamani..Hata laki mbili
    nyingikwa washukiwa Uhaini.

    Wacha Ninja na timu yake mambosasa sirro na diwani wamalize FIR RB Halafu mpka kitaeleweka.

    Musiba endelea kutumegulia WANA HEWA,
    KATKA NCHI HEWA.
    WALIOTABIRI HEWA NA KUOGELEA HEWA.
    KATIKA AWAU YA KUZIBA HEWA NA KUAZA KUHAHA KUITAFUTA MIIANYA YA KUPATA OXIJENI ILIYOZIBWA NA SAFOKESHENI ILIVYO WATIBUA WAUNZI NA KUSEMA VYUUMA VIMEKAZA..!!

    Tia girisi au wacha vikatike.

    HAPA KAZI TU MJOMBA, DAAAH.. BILIONI
    WEWE WEWE BENADI KWA KISA GANI?

    MSHAHARA MISAADA YA LIBYA LAZIMA ULUDISHE.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad