Kesi ya Lissu ya Kupinga Kuvuliwa Ubunge Kunguruma Kesho Mahakama Kuu


Kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu akipinga kuvuliwa ubunge na Spika wa Bunge, Jb Ndugai, imepangwa kuanza kusikilizwa Agosti 15, 2019 katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

Juni 28 mwaka huu, Ndugai alilitangazia bunge kuwa ameiandikia Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) kuileleza kuwa jimbo la Singida Mashariki, lililokuwa likishikiliwa na Lissu kupitia chama kikuu cha upinzani Chadema lipo wazi.

Spika Ndugai ametaja sababu kuu mbili zilizomsukuma kuiandikia tume ya uchaguzi barua hiyo, mosi ni kutokana na Lissu kutokuhudhuria bungeni kwa muda mrefu na pili kutokuwasilisha fomu ya tamko la mali na madeni kwa sekretari ya maadili kwa mujibu wa sheria.

lissu alipinga vikali kuvuliwa ubunge kwa hoja hizo alizozitoa spika Ndugai na kudai atakwenda kufungua kesi Mahakamani kwani tangu ashambuliwe kwa risasi hadi anavuliwa ubunge bado alikuwa anaendelea na matibabu.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mwakyembe...!!!
    Kuna haja ya Kuwafanyia Waandishi wetu maeneo ya Kuripoti and kuwapa atleast Crushh course.

    MWANDIKA HABARI ZA UCHUMI... AWE AMEPITIA KIDOGO ECONOMICS .

    UTAMADUNI.. AWE AMETITIA INTL CULTURE AND OUR LOCAL AFRICAN CULTURES (mILA NA DESTURI)

    Sports





    9 awe anajua kuhusu sport)
    KILIMO - AWE ANAJUA KILIMO NA TYPE NA SEASONS AJUE ANACHO KIANDIKA
    LAW NA COURT PROCEDURAL- AWE ANAJUA KIDOGO SHERIA AU AULIZE APATE UELEWA.

    AMA SIVYO ATABORONGA NA MWISHO WA SIKU KUPOTOSHA UMMA NA UELEWA WA WANAO WAHABARISHA.. KUTULETEA SINTOFAHAMU AMBAZO UNAJUA MWISHO WAKE NI SYMPATHY NA KUJIONESHA BEING VICTIMIZED.

    CHONDE CHINDE HARRISON WE NEED TO ACT.
    KUWARUDISHA SHULE NA KUWAPA VIBALI ON AREAS WHICH THEY CAN REPORT BEST. SIO KILA MSHIKA KALAMU BASI NI MWANDISHI.

    TUANZE NA LEVEL YA MA EDITOR .
    KUNA UMUHIMU

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad