Kesi ya mwandishi yashindwa kusikilizwa

Kesi ya madai ya dhamana iliyofunguliwa na mawakili kutoka Mtandao wa kutetea Haki za Binadamu (THRDC) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya mteja wao ambaye ni mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera imeshindwa kuendelea kusikilizwa baada ya upande wa washtakiwa

Wanasheria wa Mwandishi huyo waliwasilisha maombi maalum katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu siku ya jana Julai 31, ili kutaka mteja wao huyo afikishwe Mahakamani au aachiwe huru.

Akizungumza Mara baada ya kesi hiyo kuahirishwa, Wakili wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Shilinde Swedy amesema Erick Kabendera alitarajiwa kufikishwa mahakamani hapo siku ya leo ya Julai 1, lakini hakufikishwa kama mahakama ilivyoagiza.

''Upande wa mleta maombi umedai kwamba mteja wao yuko ndani kwa zaidi ya masaa 24 na dhamana ya polisi hajapatiwa, mahakamani hajaweza kufikishwa, kwahiyo Mahakama ikaamuru kwamba ni vyema zaidi kwa kuzingatia misingi ya haki, kiapo kinzani hicho kiletwe ndani ya muda mfupi ili tuweze kukisikiliza na mahakama iweze kutolewa maamuzi kwa mteja kuletwa mahakamani au kupata dhamana ya polisi'', amesema Shilinde.

Kesi hiyo ya madai ya dhamana imeahirishwa, ambapo itasikilizwa tena siku ya Jumatatu ya Agosti 5, 2019.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad