Kesi ya Ndege ya ATCL iliyozuiwa Afrika Kusini kuanza kusikilizwa

 

Maombi ya kupinga kushikiliwa kwa ndege ya Tanzania, Airbus nchini Afrika Kusini yanatarajiwa kuanza kusikilizwa hii leo na mahakama kuu nchini humo.

Akizungumzia kesi hiyo, Wakili Mkuu wa Serikali msaidizi, Dkt. Ally Posi amesema kuwa mawakili kutoka Ofisi ya Wakili Mkuu wa serikali kupitia ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali watashirikiana na mawakili wa serikali ya Afrika Kusini katika maombi ya kupinga kushikiliwa kwa Ndege hiyo.

”Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wanasimamia suala hilo, kuhakikisha Ndege hiyo inaachiwa,”amesema Dkt. Posi

Ndege hiyo ilishikiliwa kutokana na maombi namba 28/994/2019 yaliyowasilishwa na mwombaji, Hermanus Steyn kupitia ofisi ya uwakili ya Werksmans iliyopo nchini humo.

Aidha, maombi hayo ya kusikilizwa upande mmoja yaliwasilishwa Agosti 21 mwaka huu dhidi ya serikali ya Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Afrika Kusini.

Katika maombi hayo yaliambatanishwa na kiapo, kilichoapwa na Martin Richard Steyn na Bianka Pretorius wakisapoti maombi ya kuishikilia ndege hiyo kwasababu mdai anadai serikali ya Tanzania Dola za Marekani 36,375,672,81.

Mahakama ilisikiliza maombi hayo ya upande mmoja yaliyowasilishwa na mwombaji na kuamuru Ndege hiyo iwekwe kizuizini.

Mwaka 2010 mbele ya Jaji Mstaafu, Josephat Mackanja nchini humo, mdai alikuwa anadai fidia ya shamba lake jumla ya dola za Marekani milioni 36.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ngoma ni tamu.
    Temporary stay of execution order to take place and kuwafungulia shitaka la kuchafua ATCL brand na kuhatarisha Usalama wa Anga na Safety of Airplane per IOSA rules and Regulation on Operator in Accordance to EASA and FAA Board not less than $ 87 million incluging the business damageincurred duing the arbitration standoff AOG time.

    furthermore uhakiki wa wala kiapo then na Muhusika mkuu wa kesi kuwaumbua Magumashi na kuwakana mbele ya Mahakama.

    Wameumbuka wapiga Dili.

    JPM Mungu na sisi wote tuko pamoja na hivi katika Salaa ya Ijumaa tumekuombea na kuomba Allah akulinde na kukuhifadhi na Mahasidi na Vibaraka wa Mabeberu na Walowezi na Makaburu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad