Kiongozi wa Hong Kong Asema Hatajiuzulu

Kiongozi wa Hong Kong Asema Hatajiuzulu
Kiongozi wa Hong Kong Carrie Lam ameendelea kusisitiza kwamba hana mipango ya kujiuzulu katika wakati ambapo vuguvugu la wanaounga mkono demokrasia lililofanya maandamano makubwa hii leo likisababisha kuahirishwa kwa zaidi ya safari 100 za ndege na mtafaruku mkubwa kwenye usafiri.

Mapema asubuhi ya leo waandamanaji walizuia treni na milango ya kuingilia kwenye vituo na kufunga barabara na reli zinazopita chini ya ardhi.

Hatua hiyo imesababisha abiria wengi kujazana vituoni na wengine kulazimika kupatiwa huduma za dharura kutokana na kadhia hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad