Kisa wizi apewa adhabu ya kunywa ndoo mbili za maziwa


Wizi si jambo zuri hata kidogo. Ndiyo sio jambo zuri kwa sababu hurudisha nyuma maendeleo ya watu. Kuna nyakati mtu anakuwa na mali zake ambazo ameitafuta kwa tabu sana lakini mtu mmoja au kundi la watu kadhaa linaweza kumtia umasikini ndani ya muda mfupi sana.

Mara nyingi tumezoea kuona mwizi akikamatwa na watu kwenye jamii mbalimbali, watu hujichukulia hatua mkononi ama kwa kumuua kwa njia mbalimbali kama kumchoma moto au kumkata kwa vitu vyenye ncha kali kama vile panga na kadhalika

Sasa jana mkoani Iringa kuna mwizi amepewa adhabu kulingana na alichoiba. Inaelezwa aliiba ndoo mbili za maziwa zenye ujazo wa lita 20 na alipokamatwa akapewa adhabu ya kunywa na kumaliza maziwa yote yaliyomo kwenye ndoo zote mbili.



Said Kione anaesadikiwa kuiba ndoo mbili za lita 20, za maziwa fresh jana  eneo la Miyomboni, Iringa amepewa adhabu ya kunywa ndoo zote mbili za maziwa aliyoiba badala ya kupelekwa polisi baada ya kudai kuwa alilazimika kuiba kutokana na njaa na hamu ya maziwa hayo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad