Kiwanda cha Maziwa Chafungwa kwa Uchafuzi wa Mto

Kiwanda cha Maziwa Chafungwa kwa Uchafuzi wa Mto
Mamlaka ya Kuhifadhi Mazingira Nchini Kenya (Nema) imefunga kiwanda cha maziwa cha Sameer Daima kwa muda usiojulikana kwa kuchafua mtu Nairobi.

Meneja wa operesheni katika kiwanda hicho cha eneo la Viwandani jijini Nairobi, Kenneth Kareithii naye pia amekamatwa kwenye msako ulioendeshwa na maafisa wa polisi waliokuwa wameandamana na maafisa wa Nema.

Kaimu mkurugenzi mkuu wa Nema, Mamo B. Mamo ameahidi kuendelea kukabili kampuni na viwanda ambavyo vinamwaga uchafu katika mto huo wa Nairobi ambao zamani ulikuwa safi na wenye sifa nzuri.

Maafisa wa Nema pia wamefanya msako katika kampuni ya kemikali ya Synresins inayotengeneza malighafi muhimu katika kutengeneza rangi, wino na vitambaa na kumkamata Afisa Mkuu Mtendaji Mira Shah, meneja wa uzalishaji bidhaa Michael Mungai na mkuu wa nguvukazi Yvonne Nyokabi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad