Kocha wa YANGA Ajitapa Mchezo wa Kwanza Leo na RUVU Shooting...Njooni Muone Kazi ya Wanaume



MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ameandaa dozi maalum kwa ajili ya Ruvu Shooting mchezo utakaochezwa leo Uwanja wa Uhuru.

Akizungumza na Championi Jumatano, Zahera alisema kuwa amewaambia wachezaji wake wote kuwa mchezo wa kwanza ni muhimu kwao kushinda.

“Tunaanza rasmi ligi kwa kucheza na Ruvu Shooting siyo timu ya kubeza kwa kuwa ipo ndani ya ligi, nimewaambia wachezaji wangu ni lazima tuwape dozi maalum wapinzani wetu kujiweka kwenye mazingira bora msimu huu.

“Tuna kazi ngumu kimataifa hilo lipo wazi lakini ndani ya ligi pia ni muhimu na niliwaambia awali kwamba tunakuja kupambana kutwaa taji la ligi na safari ndiyo inaanza kwa sasa,” alisema Zahera.

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, alisema kuwa kikosi kipo salama na wanachohitaji ni pointi tatu muhimu.

Stori na Lunyamadzo Mlyuka Dar es Salaam
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad