Kuhusu Penzi la Siri la DIAMOND na Menina....Kutoendana Kimuonekano ilikuwa Tatizo

Fahamu: Diamond Platnumz aliwahi kumfukuzia Menina muda mrefu hadi kwenda kujitambulisha nyumbani Kwa kina Menina ili amuoe lakini actress, MC na muimbaji huyo aliyeanzia Bongo Star Search alikataa. .

Mwaka 2014 wakati media zikiwa zimeshupalia kuwaandika kuwa ni wapenzi, Menina alikaririwa akisema ni kweli Mond alijitambulisha Kwao kutaka kumuoa lakini amekataa kwakuwa yeye Menina alikuwa na mchumba tayari muda huo, pili Meninah alisema alikuwa anamheshimu sana wema Sepetu ambaye muda huo alikuwa mpenzi rasmi wa Diamond, tatu Menina alidaiwa kusema yeye na Mond hawaendani kabisa kimuonekano .

Ingawa Media zilishupalia kuwa Menina na Mond wanatoka Kwa siri, Kisha Menina na Mond kukana. Lakini baada ya muda mrefu kupita Wema Sepetu aliibuka kuwaambua Menina na Diamond kuwa ni waongo akisema Ni kweli walishatoka kimapenzi. Wakati wema alipoulizwa na GPL kama anaweza kukubali kuolewa na Diamond au hatakubali? wema alijibu .

"Ilikuwa zamani , sio sasa hivi kwa sababu nasibu nimekaa nae sana kwa muda wa miaka miwili .najua alivyo na hatanisumbua sana kwa sababu mimi nilimwacha CK kwa ajili yake lakini matokea yake alikuja akatoka kimapenzi na meninah na meseji nilizibamba.kwahiyo hata kwenye ndoa hawezi kubadilika , yuko hivyo"

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad