Kuna ubaya wanawake kuvaa vikuku? Mtazamo wa Kiislamu


Watu wengi wamekuwa na mtazamo hasi juu ya wanawake kuvaa urembo wa cheni miguuni maarufu kama ‘Vikuku’ kwa kuuhusisha urembo huo na ishara ya uhuni au tabia mbaya kwa wanawake.

tetesi hizo zimekua zikileta mkanganyiko kwenye urembo huo, na kusababisha wengi kuuchukia na wengine kukataza kabisa watu wao wakaribu wasithubutu kuvaa.

tukiachana na mitazamo hiyo mbali mbali, ambayo naamini hata wasomaji humu mna mitazamo yenu juu ya vikuku, tujifunze kidogo mtazamo wa waislamu iwapo kuna ubaya wowote kwa mwanamke kuvaa kikuku.

Picha inayohusianaUkurasa waKiislamu wa Alhidaaya unaeleza kuwa hakuna ubaya kwa mwanamke kuvaa mkufu miguuni ikiwa ni kwa ajili ya kujipamba kwa mumewe. Na wala asidhihirishe mapambo hayo nje kwa wasiomhusu, yaani wasio maharimu zake.

Dalili ya ukweli juu ya hilo inapatikana katika Aaya ya hijaab inayomalizia kukataza wanawake wanaovaa mikufu miguuni mwao wasitembee kwa kupiga miguu yao hadi ijulikane kuwa wamevaa mapambo hayo miguuni mwao:

 ((وَلَا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِن زِينَتِهِنَّ))

((Wala wasipige chini miguu yao ili yajulikane mapambo waliyoyaficha)) [An-Nuur: 31]

Picha inayohusianaHii ni wazi pia kuwa hijaab ya sheria inampasa mwanamke ajifunike hadi miguuni mwake. Tunaona dada zetu wengi wanajifunika tokea juu lakini miguu yao iko wazi hata katika Swalah utawaona wanaswali na miguu, vidole vya miguu vinaonekana.

Swalah zao hawa zinakuwa hazikukamilika kwani mwanamke anatakiwa ajifunike kote isipokuwa uso tu na viganja vya mikono.

Na Allaah Anajua zaidi

Chanzo: www.alhidaaya.com
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad