Kwa Kapombe lazima upambane buana!


JE unataka kufikia mafanikio ya beki wa Simba, Shomary Kapombe na hujui ufanye nini? jamaa ameweka wazi siri ya mafanikio yake kwamba mazoezi na nidhamu ndio silaha ya kumfanya kiwango chake kiendelee kuwa bora.

Pamoja na kuwepo mabeki ambao wanatamani kufika hatua yake, Kapombe anasema anajifunza kila siku ili kuhakikisha anaendana na soka la kisasa litakalomfanya afike mbali zaidi ya alipo kwa sasa.

Anaeleza kwamba anazingatia mazoezi nakuyafanya kuwa sehemu ya maisha yake anapokuwa kambini na nyumbani, akidai yanakuwa yanamuandaa kwa ajili ya mwili wake kuwa tayari kwa kazi inayokuwa mbele yake.

“Mchezaji akiwa mvivu wa mazoezi ni ngumu kuwa na vitu muhimu vitakavyokuwa vinaipa thamani kazi yake, kama kuwa fiti, akili ya mchezo, kasi na pumzi, hivyo vyote vinapatikana kwa kuzingatia mazoezi ya nguvu,” anasema mchezaji huyo.

“Huwa sipendi kusukumwa na kocha kufanya mazoezi, napenda kujituma mwenyewe hilo linanisaidia kazi yangu kuiona ni rahisi na naifurahia kuifanya kwa moyo wote ndio maana nikiwa uwanjani natamani kufanya zaidi ya majukumu yangu.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad