Kijana, Epuka Mwanamke Aliyeharibika Akili Usijejuta


Ni kasumba iliyoshamiri siku hizi vijana kujichanganya na kuoa mabininti ambao kimsingi wameharibika. Tabia zao si za mke wa ndoa tena wana sifa zote za usela. Unapooa mwanamke wa sampuli hii unajijengea kaburi lako mwenyewe kwani huna uwezo wa kumbadilisha ama yeye mwenyewe kubadilika. Utawatambuaje wanawake walioharibika? Hizi hapa baadhi ya dalili zao:

1. Mwenye tattoo
Ni rahisi kuhoji tattoo ina uhusiano gani na tabia ya mtu, lakini ukweli ni kwamba binti yeyote anayejiheshimu na kuheshimu maadili hawezi kamwe kujichora tattoo mwilini. Hiki ni kielelezo cha binti aliyeharibika na kujiona ni wa kisasa zaidi na kuwa ni msela, unapojichanganya na huyu uwe na hakika umejimaliza mwenyewe. Kama unabisha angalia mabinti wamejichora mitattoo ya ajabu mpaka kwenye vinena vyao, ni binti asiyejitambua pekee anayeweza kufanya ujinga huu.

2. Ametoga matundu kumi sikioni na kwenye pua
Naomba nieleweke hapa, kuna mila ambazo mwanamke kutoga pua ni urembo, hata masikio pia. Lakini kwa binti wa sasa kutoga matundu meengi masikioni utadhani ng'ombe au kutoga matundu mengi puani mpaka inakuwa kinyaa ni dalili za kuharibika akili.

3. Amewahi kuwa na wapenzi zaidi ya wawili
Hapa ni kama umeshindwa kumpata bikra, mwanamke walau basi awe amewahi kutoka na mpenzi mmoja, ikizidi sana wawili. Huyu anaweza kuwa mshamba wa mapenzi bado, hivyo huenda akatulia. Zingatia kwamba hii ni bahati nasibu, itategemea mambo mengine mengi ili kuhakikisha hili. Lakini mwanamke aliyekwenda na zaidi ya wapenzi wawili elewa wazi kuwa huyu amezibuka, ni mzoefu na ana staili anazozipenda. Sasa uwe tayari kumpa hizo staili vinginevyo jiandae kisaikolojia.

4. Yuko tayari kuse.x nawe siku ya kwanza kukutana
Yaani binti unakutana naye siku ya kwanza na yuko tayari kwenda kitandani!! Unataka uone nini tena ndipo ujue umeuvaa mkenge? Huyu lazima atakuwa kiruka njia tu, hamna namna nyingine ya kumwelezea.

5. Amelelewa na Single mother
Binti mwenye maadili ni lazima apate malezi ya pande zote mbili. Ni hatari sana kwa binti kulelewa na mama tu, kwani hakutakuwepo na uwiano. Mara nyingi mabinti wa aina hii huwa na ukosefu wa maadili kwa sababu ya mapungufu ya upande mmoja. Wengine hufundishwa kuwachukia wanaume na kuwa washindani badala ya partners. Ni kujitakia ugonjwa wa moyo kuoa binti ya aina hii.

6. Ana matatizo ya akili
Ukiingia kwenye uhusiano na binti akaanza kukuelezea matatizo ya akili yanayomsibu nyakati fulani ni dalili kwamba unakaribisha matatizo kwenye ndoa. Kama wewe ni nicce guy unaweza kumchukua ili ukamtibu, lakini mpaka kufikia umri alionao maana yake tayari akili ishapata hitilafu.

7. Ana maisha ya kisela
Binti ambaye amekuwa akiishi ghetto ama nyumbani kwao lakini anahusudu maisha ya kisela, anavaa nguo za ajabu ajabu, anaambatana na makundi ya wasela, muepuke kama ukoma. Binti wa namna hii hana malengo ya familia na maishani mwake anaona kula bata ndio kila kitu. Utajikuta unasimama peke yako kwenye malengo yako na hata malezi ya watoto atakaokuzalia.

8. Anapenda pesa
Je, mpenzi wako kakugeuza ATM? Basi kimbia upesi, haupo mahali salama. Mwanamke mwenye mapenzi ya kweli ataonyesha nia ya kushirikiana tangu hatua za awali. Hata pale anapogundua umepungukiwa ama umepigika, atajaribu kukukwamua pale anapoweza, anajisikia fahari kukusaidia ufanikiwe mambo yako, anahesabu mafanikio yako kuwa ni yake. Kama mwenza wako anakuja na mahitajio ya pesa kila sekunde kiasi kwamba unajiona kama huna vya kutosha kujibu mahitaji yake, umepatikana. Kimbia upesi!!

Kwa nini uwaepuke?

1. Hawatabiriki
Unapotaka kuoa unahitaji kujenga familia, watoto wasome mpaka chuo uwaandalie maisha yao ya baadaye, familia iishi maisha mazuri n.k. Ukioa mwanamke huyu atayapasua malengo yako na kujikuta ukiyumba. Unahitaji partner, mshirika, ambaye mtakuwa na nia moja, atakayetumia nguvu zake kuwalea watoto na kukusaidia kufikia malengo ya maisha.

Kuna nyakati utapambana na hali ngumu ili kufikia malengo, mwanamke asiyetabirika anaweza kuwa kinyume nawe tofauti na matarajio yako. Unapaswa kuwa na mwanamke atakaye kuwa bega kwa bega nawe katika nyakati zote.


2. Atakulazimu uelekeze nguvu na malengo kwake kuliko kwenye malengo ya maisha
Mwanamke aliyeharibika atakugeuza jibu la matatizo yake. Atataka utumie nguvu zako zote kutatua matatizo aliyoingia nayo kwenye ndoa, yawe binafsi ama ya wazazi, ama ndugu wa karibu akitafsiri kwamba huu ndio upendo kwake. Atakutoa kwenye malengo yako na kukuelekeza kwenye malengo tofauti kabisa.

☆ Nice guys mara nyingi huumizwa sana na hawa wanawake. Kwa nini? Kwa sababu wanajaribu kuwaokoa wanawake hawa walioharibika, matokeo yake huvutwa chini na wanawake hawa badala ya kwenda juu. Wanawake hawa huwashusha chini katika malengo yao, na bahati ni pale wanapoishia kuwashusha tu. Kwani wengine huwazamisha kabisa hawa mr nice guys!`
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad