Lori Lingine la Mafuta Lapinduka Kagera, watu Wachota Mafuta Kama Kawa



Wakati bado Watanzania wakiendelea kuomboleza vifo vya zaidi ya watu 100 kufuatia ajali ya moto Morogoro iliyotokana na mlipuko wa lori la mafuta, baadhi ya Wananchi wa Kagera wamejitokeza kwa wingi kuchukua mafuta kwenye ajali ya Lori la mafuta lililoanguka jana eneo la Benako Ngara Mkoani Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti amenukuliwa na mtandao wa Millard Ayo akisema ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani humo kufanya msako mkali na kuwakamata wote waliochota mafuta na kuwafikisha kwenye mikono ya sheria.

Katika video inayosambaa mtandaoni inaonesha watu kadhaa bila hofu yoyote wakiwa wanachota mafuta kwa na kuweka kwenye madumu, jambo ambalo ni hatari ikiwa kutatokea mlipuko.

Matukio ya namna hii yamekuwa yakitokea sehemu mbalimbali nchini lakini yamewahi kusababisha athari kubwa kwenye mikoa ya Morogoro ambayo bado haijasahaulika kutokana na kuua na kujeruhi watu wengi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad