Maalim Seiff akamiwa kuumbuliwa, sakata la gari za CUF ngoma mbichi.
0
August 11, 2019
Na Ahmad Mmow, Lindi.
Sasa nidhahiri hali sio shwari baina ya CUF-Chama Cha Wananchi( CUF ) na ACT-Wazalendo. Baada ya CUF kumtaka aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho, Seiff Shariff Hamad (Maalim Seif) na watu wengine waliohama na mali za chama hicho warejeshe mali hizo kwa hiari yao badala ya kusubiri kuumbuka.
Onyo hilo lilitolewa jana mjini Lindi, na katibu wa CUF wa wilaya ya Lindi vijijini, Mohamed Shadhily alipozungumza na waandishi wa habari kukanusha taarifa ya viongozi wa mkoa wa Lindi wa ACT-Wazalendo ambao siku chache zilizopita walisema waliporwa gari na walinzi wa CUF.
Shadhily alisema licha ya kuchukua gari hiyo kutoka kwa baadhi viongozi ya wa mkoa wa ACT-Wazalendo katika kijiji cha Nachunyu, wilaya Lindi, wataendelea kurejesha mali za chama chao kutoka popote zilipo.
Alisema gari waliyochukua katika kijiji hicho ni miongoni mwa gari sita zilizokuwa zinatafutwa. Hata hivyo gari tano zilizokutwa zimefichwa Dar-es-Salaam walichukua, ikabaki hiyo iliyokutwa kijijini Nachunyu.
'' Hao viongozi wa ACT wanaudanganya umma, kwani mimi tarehe 6.8.2019 nilitoa taarifa polisi kituo cha Lindi kwamba gari hiyo imeonekana katika wilaya hiyo. Kwahiyo tunakwenda kuchukua, iwapo kutakuwa na ugumu tutahitaji msaada wa jeshi hilo. Kwabahati nzuri walitukabidhi wenyewe baada ya kuondoa vitu vyote vilivyokuwa ndani ya gari hiyo,'' alisema Shadhily.
Katibu huyo alisema taarifa ya kupatikana gari hiyo wamepeleka katika kituo cha polisi Buruni ambako waliliripoti kutoroshwa kwa gari hizo, makao makuu ya CUF na kwa mkuu wa jeshi la polisi (IGP).
Licha ya kukiri kwamba kadi ya gari hiyo inaonesha ni mali ya Nassoro Mazrui, lakini alisema kwenye orodha ya mali ya chama iliyopo kwa msajili wa vyama vya siasa ni pamoja na gari hiyo.
'' Hiyo imetokana na udhaifu wa Maalim Seiff ambae aliwamilikisha watu mali za chama kwamadai kwamba zingesajiliwa kwa jina la chama, kingehujumiwa na serikali. Hizo zinazoonesha kuwa nizawatu ndizo kwa msajili zinaonesha ni mali ya chama, na maalim ndiye aliyepeleka orodha hiyo kwa msajili,'' alisisitiza Shadhily.
Katibu huyo ambae alikiri kuratibu mpango wa kuchukua gari hiyo kutoka mikononi mwa viongozi hao wa ACT alitahadharisha kwamba wataendelea kurejesha mali zao popote zilipo. Huku akionya kwamba muda mfupi ujao watakwenda kuchukua gari 22 zilizofichwa visiwani Zanzibar.
Alisema kutokana na kuwa na uhakika wa mahali zilipofichwa, urahisi wa kufikika na uwezo wakuchua, alitoa wito kwa wote waliohama chama hicho, akiwamo Maalim Seiff kama wanamiliki mali za chama hicho warejeshe kwa hiari baadala ya kusubiri kuendelea kuumbuka.
Tags