Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtaka mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewj kuendelea kuwekeza nchini na kuitangaza nchi.
Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kusaga nafaka kilichopo chini ya Kampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited (MeTL).
Rais Magufuli amemtaka mfanyabiashara Mohamed Dewj kutokukubali kurudishwa nyuma na baadhi ya watendaji watakao jaribu kuweka vikwazo kwa wawekezaji.
”Mo’ Dewj wewe ni bilionea kijana Afrika, chapa kazi, usikubali akukwamishe mtu, uwekezaji huu ni mkubwa sana, kwa hiyo Tanzania iko pamoja na wewe,”amesema Rais Magufuli
Aidha, Rais Magufulia amewataka watendaji walioko ndani ya serikali kutowavuruga wafanyabiashara ambao wamekuwa wakiwekeza nchini na kuongeza pato la taifa.
Hata hivyo, Rais Magufuli ametumia nafasi hiyo kumuagiza Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa kuwachukulia hatua watendaji wa wizara yake wanao wakwamisha wawekezaji.