Mahakama Yaelezwa Mwandishi Erick Kabendera Amepooza Mguu Mmoja na Ana Tatizo la Kupumua
0
August 30, 2019
Dar es Salaam. Upande wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mwandishi wa habari nchini Tanzania, Erick Kabendera, wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kulielekeza Jeshi la Magereza mteja wao kwenda kupimwa katika hospitali ya Serikali.
Wakili wa utetezi, Jebra Kambole amedai leo Ijumaa Agosti 30, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Mtega baada ya Wakili Mwandamizi wa Serikali Wankyo Saimon kueleza upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika wakati kesi hiyo ilipotajwa.
Wakili Kambole amedai usiku wa kuamkia Agosti 2, 2019 mteja wake akiwa gerezani alianza kuumwa na hadi leo ana shida ya kupumua.
"Nilienda kumuona nikakuta amepooza mguu na kushindwa kutembea kwa siku mbili pamoja na kuishiwa nguvu, sisi kama mawakili na ndugu hatujui nini anachoumwa."
"Kwa kuwa mteja wetu hajapata vipimo ambavyo vinastahili tunaomba Mahakama ielekeze Jeshi la Magereza mteja wetu akapimwe katika hospitali yoyote ya serikali ikiwemo Muhimbili penye vipimo vya uhakika," amedai Wakili Kambole
Wakili Wakyo amedai swala la ugonjwa hakuna mtu anayeweza kupingana nalo lakini huwezi kulielekeza Jeshi la Magereza kwenda kumpima katika hospitali fulani
Mwananchi
Tags