Maiti zaidi ya 26,000 zakosa ndugu wa kuwazika

 

Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez amesema kwamba serikali yake inakabiliwa na changamoto ya kufumbua kitendawili cha maiti zaidi ya 26,000 ambayo haieleweki ilikotoka. 


Kwenye taarifa yake kwa umma hapo jana, Rais Lopez alisema kuwa serikali yake imeipa kipaumbele shughuli ya kutambua maiti hizo. 


 “Uhalifu, mauaji na watu kupotea kila mara hapa nchini ni baadhi ya changamoto tunazokabiliana nazo hapa,” Lopez alisema. 


Aliongeza kwamba maafisa wa serikali yake wanajitahidi kutambua maiti hizo 26,000 ambazo zinaleta msongamano kwenye vyumba vya kuhifadhi maiti kwote nchini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad