Mkuu wa mkoa wa DSM Paul Makonda leo alimtembelea Ashraf Hamza ambaye alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili kutokana na tatizo la uvimbe katika eneo lake la uso lililokuwa akikabiliana nalo.
Katika mazungumzo yake Makonda ameridhishwa na huduma iliyotolewa na Hospital hiyo Taifa kwani wamesaidia kuleta nafuu kwa Ashraf ambaye anaendelea vizuri kwa sasa.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amewataka watanzania kuona umuhimu wakuwa na bima ya afya kwani itawasaidia pindi wapatapo shida ya kiafya.