Makonda alalamikia hujuma ufukwe wa Coco


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, ametoa mwezi mmoja kwa Manispaa ya Kinondoni kuanza ujenzi wa mradi wa ufukwe wa Coco Beach, kwa kile alichokidai Manispaa hiyo imekuwa ikichelewesha mradi huo.


Paul Makonda ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam, wakati alipotembelea eneo la ufukwe wa Coco Beach, ambapo amesema Manispaa hiyo imekabidhiwa Bilioni 14, lakini mpaka sasa wanaishia kufanya vikao tu.

"Eneo hili la Coco Beach limerudishwa kuwa eneo la umma, ili watu waje kupumzika, Rais akatoa bilioni 14, ili kuanza kuijenga Coco, masikitiko yangu mpaka sasa ujenzi haujaanza." amesema Makonda

"Moja ya mambo yaliyonishangaza ni mshauri waliyempata ameacha mchoro wa bilioni 14, amekuja na mchoro wa bilioni 40, tumewapa muda wa mwezi mmoja ili Coco Beach ianze kujengwa, haiwezekani fedha imetolewa miradi haiendi, natoa mwezi mmoja muanze kushughulikia" amesema Makonda.

Katika ziara hiyo Makonda amewataka viongozi wa Manispaa ya Kinondoni kuendana na kasi ya ujenzi wa daraja la Selander, ambapo amependekeza mpaka mradi wa daraja hilo kukamilika na uboreshaji wa ufukwe wa Coco Beach uwe umekamilika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad