Mama mzazi was Mwandishi Erick Kabendera Atofautiana na Polisi Kuhusu Uraia wa Mwanawe


Mama ya mwanahabari Eric Kabendera, Verdiana Mujwahuzi, 80 amezungumza na wanahabari kwa mara ya kwanza tangu mwanawe akamatwe Jumatatu wiki hii na maafisa ambao hawakuwa wamevalia sare rasmi za polisi.

Tayari kamanda wa polisi kanda maalum ya mji wa Dar Lazaro Mambossasa amethibitisha kuwa mwandishi huyo alikamatwa kuhusiana na utata unaokumba uraia wake.

Lakini mama Mujwahuzi anapinga kauli ya polisi kuhusu uraia wa mwanawe.

''Kabendera ni mwanangu, nilimzaa hapa Tanzania na hapajawahi kuwa na utata kuhusu anakotoka, polisi iseme ukweli inamshikilia kwa nini'' aliliambia Gazeti la The Citizen nchini Tanzania.


Kwa mujibu wa Gazeti hilo mama huyo wa miaka 80 alikuwa nyumbani kwa mwanawe tukio la kukamatwa kwake lilipotokea.

''Nimejawa na wasiwasi na hakuna yeyote anayenipatia habari kumhusu'' alisema mama Mujwahuzi akihojiwa na The Citizen.

Mama huyo haelewi kosa alilofanya mwanawe ni lipi na haamini ikiwa suala la yeye kuwa Mtanzania au la.

Pia anataka kujua nia ya serikali kumhoji uraia wa mwanawe akisisitiza kuwa ni Eric ni raia wa nchi hiyo kwa kuzaliwa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad