Mambosasa Apiga Marufuku Ving'ora vya Magari Haya

Mambosasa Apiga Marufuku Ving'ora vya Magari Haya
Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar Es Salaam SACP Lazaro Mambosasa, amepiga marufuku uwekaji wa Alarm, Ving'ora na Sports light kwenye magari ya watu binafsi kwani vinasababisha taharuki kwa watumiaji wengine kuhisi kuna msafara wa kiongozi au mgonjwa.


Kamanda Mambosasa ameyabainisha hayo leo Agosti 5 ikiwa ni kipindi cha Mkutano wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC na kwamba kuanzia kesho Agosti 6 msako mkali utaanza kufanywa na kuwakamata watakaokaidi agizo hilo na  ni marufuku ya kudumu.

''Marufuku hiyo inakwenda kwa watu wote wenye magari waliyoweka alarm, isipokuwa kwa magari maalumu kama polisi na Ambulance, msako mkali unaanza kesho yeyote atakayekamatwa na hizo taa iwe urembo lakini unasababishia watu taharuki na kupaki magari na kunyimwa haki ya kutumia barabara, watakamatwa na sitowaachia mpaka watakapokuja na mafundi wao waje kuwabadilishia kituoni.'' amesema Mambosasa.

Kwa upande mwingine jeshi la polisi limepiga marufuku kwa madereva bodaboda wote, kufika mjini kwa kipindi hiki chote cha ugeni na kushauriwa waendelee kufanya biashara zao pembezoni mwa mji.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad