Maneno ya Samatta baada ya kufunga ‘hat-trick’ yawaibua Manara, Salim Kikeke na Profesa Jay


Mshambuliaji hatari wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta tarehe 17/08/2019 wikiend hii ilifanikiwa kuipatia klabu yake ya KRC Genk jumla ya mabao matatu (Hat-Trick) kwenye mchezo ambao timu hiyo iliibuka na jumla ya ushindi wa mabao 4 – 0 dhidi ya Waasland-Beveren (WBE) mechi ya ligi.
Mchezaji huyo hatari na moto wa kuotea mbali, Samatta alifunga mabao hayo kuanzia dakika 51′, 66′ na 86 wakati la nne likifungwa na kiungo  wa Ghana Joseph Paintsil.

Siku moja mara baada ya kufunga mabao hayo Samatta aliandika ujumbe unaoeleza furaha yake kupitia akaunti yake ya Instagram.

”Ni furaha kupata point 3 muhimu Leo nje ya nyumbani, timu ilicheza vizuri. Na tunawashukuru mashabiki waliosafiri kutupa sapoti. Forza genk🔵⚪ Pia nna furaha kufunga hattrick yangu ya kwanza msimu huu naimani nyingi zitakuja 😁  Am proud of the boys.  Captain diego🧔🏾.” Aliandika Mbwana Samatta kupitia akaunti ya Instagram.

Mara baada ya kuandika ujumbe huo Samatta ameweza kupata mchango wa mawazo kutoka kwa Watanzania mbalimbali wakiwemo watu maarufu kama Mtangazaji wa Shirika la habari la BBC, Salim Kikeke, Haji Manara, Rapper Profesa Jay ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Mikumi na watu wengine.

Na hivi ndivyo walivyochangia ujumbe wa Mbwana Samatta, hasa kwakutaka kuongeza juhudu pamoja na kumsia.

salim_kikeke
Verified
Left foot, right foot header! Knock ‘em out! 👊🏿👊🏿👊🏿

hajismanara
Verified
🙌🙌

professorjaytz
Verified
Tunaaanzaa upyaaaaaaaaa🙌🙌🙌

samagoal77
Verified
@professorjaytz mwanzo kabisa

jerrymuro1980
Sisi tunaendelea kukuombea , kwa sasa tunaona hapo sio mahali pako, wameshakuelewa sana uwezo wako cha msingi sasa tuondoke hapo twende mbele kaka yangu hao wakikuzoea watadhani unafanana nao wakati wewe ni level ingine @samagoal77

official_juma_kaseja
🔥🔥🔥🔥🔥🔥💪💪💪💪💪 @samagoal77

himid23mao
Verified
Diego 🧔🏽 👊🏽⚽️💪🏽

samagoal77
Verified
@himid23mao zizou
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad