Maswali sita ya Majaliwa kuhusu ajali ya moto iliyoua 69 Morogoro


Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameuliza maswali sita kuhusu ajali ya moto iliyoua Watanzania 69 mkoani Morogoro huku akitangaza kuunda kamati kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa ajali hiyo.

Ajali hiyo ilitokea jana Jumamosi Agosti 10, 2019 katika kijiji cha Itigi, Msamvu mkoani Morogoro   baada ya lori la mafuta kupinduka na kuwaka moto muda mfupi baada ya watu kuanza kuchota mafuta.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza katika uwanja wa shule ya sekondari Morogoro kwa ajili ya kuaga miili ya waliokufa katika ajali hiyo, Majaliwa ameitaka kamati hiyo kutoa majibu Ijumaa Agosti 16, 2019.

Picha za video zinaonyesha lori hilo likiwa limepinduka barabarani na mafuta yakichuruzika kuelekea pembeni mwa barabara ya Morogoro- Dar es Salaam ambako watu waliokuwa na madumu ya ujazo mbalimbali walikuwa wakichota mafuta kabla ya moto kuwaka.

Akizungumza kwa mtindo wa kuuliza maswali, Majaliwa alianza na swali la kwanza na kusema, “Ajali ilipotokea kila mmoja kwa majukumu yake aliwajibika?”

Katika swali la pili amesema, “Ajali ilipotokea ni mahali palipo na shughuli nyingi za kijamii ikiwemo kituo kikuu cha mabasi tuna trafiki hapo, tuna polisi wa ulinzi hapo. Ilipoanguka tu nani alitokea wa kwanza.”

Mwananchi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad