Mawakili wanne wanatarajiwa kuanza kumtetea aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyevuliwa wadhifa huo hivi karibuni.
Lissu yuko nchini Ubelgiji alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu ambao hadi sasa hawajajulikana, alifungua rasmi shauri hilo jana.
Alute Mughwai kaka yake Lissu akizungumza na waandishi wa habari amesema kesi hiyo itaanza kuunguruma Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.
Mawakili hao wataongozwa na Kibatala na wengine ni Jeremia Mbesya, John Malya na Fredi Kalonga.
Amebainisha kuwa maombi ya kufunguliwa kesi hiyo chini ya hati ya dharura, kupitia kwake (Mughwai) aliyempa mamlaka ya kisheria kufanya hivyo, yatasikilizwa Agosti 21, 2019.
Mughwai amesema wanatarajia Lissu kurejea Tanzania Septemba 7, 2019 baada ya uchunguzi wa mwisho wa madaktari wake utakaofanyika Agosti 20, 2019.
Ndugu wanahabari wenzangu. Kwa heshima naweledi wa kazi zetu.
ReplyDeleteHuyu mssaliti aliye ipaka Matope na anaendelea hivyo anacho taka kwa sasa ni kuwa Mitandaoni na Magazetini.
Naomba Tumchunie..!!!
Kama ni kesi basi watanzaania wengi wanazo na wala hatuzisikii wala kuziona na yake kama itatupiiwa mbali
au kusikilizwa na kufungwa manake ni kwa maombia ya hati ya Dharura. Ambayo kila Mtanzania ana haki nayo na nyigi hufungwa naa kutupiliwambali baada ya kukosa mashiko na mapungufu ya kisheria katika Uwasilishaji.
Naomba kwetu sisi tuwe na weledi na kujua tunacho taka kuandika kwa uelewa japo mdogo kama inabidi kuandika.
Mdau uko sahihi,
DeleteAatakakula hela za Dezo za Walipa kodi.
Ndugai ameamua kwa Wabunge Hewa kuzkiatia na kuziba Hewa.
nchi iikwa pabaya..!
₩afanyakazi Hewa
Wanafunzi Hewa
Pembejeo Hewa
Kaya maskini Hewa
Mikoppo Hewa
Wabunge Hewa (Lissu umeshtukiwa)