Mbunge aingia na mtoto Bungeni, atolewa


Zulekha Hassan ambaye Mwakilishi wa wanawake eneo la Kwale kwenye Bunge la Kenya, amefukuzwa bungeni baada ya kuingia akiwa na mtoto tukio ambalo lilisababisha shughuli za Bunge kusimama kwa muda.

Mama huyo amesema, mtoto huyo wa kike ambaye bado ananyonya ni wa tatu kwake tangu awe Mbunge mwaka 2013 na hajawahi kuingia na mtoto bungeni kama alivyofanya leo.

Mbunge huyo amesema, dharura imesababisha aingie bungeni na mwanawe kwa sababu bado ananyonya na ilibidi achague au kutokwenda kazini au kwenda ukumbini na mtoto hivyo hakuona sababu ya kutofanya kazi kwa sababu ya mtoto.

"Nimekuwa hapa, hiki ni kipindi changu cha pili, nimekuwa Mbunge tangu mwaka 2013, huyu ni mwanangu wa tatu, leo tupo na emergency (dharura), ilibidi nifanye hivyo sikuwa na namna nyingine, na niliwaza kwa nini nisiende kazini kwa sababu nitaadhibiwa kwa kuwa na mtoto na ni jambo la asili kabisa," amesema nje ya ukumbi wa Bunge jijini Nairobi.

Amesema, kwenye eneo hilo hakuna eneo maalumu kwa ajili ya wabunge au wafanyakazi wa Bunge kuweka watoto hivyo hakuwa na namna nyingine zaidi ya kuingia ukumbini na mwanawe.

Kwa mujibu wa Mbunge huyo, mwaka 2013 Tume ya Utumishi wa Bunge iliagiza kuwe na chumba ili wabunge na wafanyakazi wa Bunge wakitumie kunyonyesha watoto na kuwaweka huko lakini hadi sasa hili halijatekelezwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad