Mbunge CCM atangaza kung’atuka, ‘Sasa ni zamu ya vijana’


Mbunge wa jimbo la Rorya kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Lameck Airo amesema kuwa hatogombea tena katika uchaguzi mkuu ujao na badala yake atawaachia vijana.

Amesema kuwa ingawa hatagombea tena lakini atatimiza ahadi zake zote alizoahidi wakati wa kampeni za mwaka 2015 na kwamba kwa kazi aliyoifanya ndani ya miaka tisa itabaki kuwa historia.

Ameyasema hayo wakati wa ziara yake akiwa jimboni mwake, ambapo amesema kuwa tayari ameshakijulisha chama chake juu ya kusudio lake la kutaka jimbo la Rorya liongozwe na vijana shupavu na wenye sifa.

”Kama Mbunge nitahakikisha kwa kipindi kilichobaki cha mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu, ahadi zangu zote zinatekekelezeka ili atakayerithi  nafasi hii chama kisipate shida 2020,”amesema Airo

Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM wilaya ya Rorya, Charles Ochele amethibitisha mbunge huyo kutoa taarifa ya kutogombea tena 2020 huku akisema kuwa haitakuwa jambo la kushangaza endapo atabadili mawazo ya siku za mbeleni.

Hata hivyo, Ochele amesema kuwa Airo ni mbunge wa mfano katika jimbo hilo kutokana na maendeleo aliyoyafanya kwa kuwaondolea wananchi kero mbalimbali zilizokuwa zikiwakabiri hapo awali.

Dkt. Bashiru Ally awacharukia wakuu wa mikoa, ‘mjitafakari’
Upinzani wang’aka, ‘Hatususii uchaguzi’
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad