Membe Atoa Neno Kuhusu Kushikiliwa kwa Kabendera

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe ameungana na baadhi ya Watanzania katika kampeni ya ‘Free Kabendera’ ambayo inalenga kupata kura takribani laki moja ili kutoa msukumo kwa mwandishi Erick Kabendera kuachiwa huru.

Jana Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe alihamasisha Watanzania kuungana kwa pamoja ili mwandishi huyo aachiwe huru.



Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Membe amesema anaungana na Mama mzazi wa mwandishi huyo na baadhi ya Watanzania kupaza sauti yake kuomba serikali imwachie huru.



Bernard K. Membe
@BenMembe
Please Free Eric Kabendera! Niungane na Mama mzazi wa Eric na Watanzania wengi kupaaza sauti yangu kuomba Serikali imwachie huru Eric bila masharti yoyote.Tanzania ni nchi kubwa na sifa moja ya nchi kubwa ni kutenda haki na kukumbatia press freedom. Choonde!


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jumatatu Agosti 5 ilimsomea mashtaka matatu Kabendera ambayo ni kujihusisha na genge la uhalifu na uhujumu wa uchumi, kukwepa kulipa kodi ya zaidi ya milioni mia moja za kitanzania pamoja na utakatishaji fedha zenye thamani ya zaidi ya millioni mia moja na sabini.



Kwa mujibu wa mashtaka yaliowasilishwa, Kabendera anadaiwa kuyatekeleza hayo baina ya Januari 2015 na Julai mwaka huu mjini Dar Es Salaam na kwa baadhi ya makosa anadaiwa kuyafanya kwa ushirikiano wa watu ambao hawakuwepo mahakamani leo.

Makosa yote hayana dhamana.

Wengine ambao wameonaka kufanya kampeni hiyo ni Zitto Kabwe, Godbless Lema, Maria Sarungi na wengine baadhi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad