
DJ Arafat amefariki akiwa na umri wa miaka 33 na alipata umaarufu sana kutokana na style yake ya kipekee kwenye muziki ambayo amekuwa akiifanya na hata kushirikishwa kwenye kolabo mbalimbali na wasanii tofauti tofauti ndani ya bara la afrika.
Mpaka umauti unamfika DJ Arafat alikuwa ni miongoni mwa wasanii waliokuwa wanawania tuzo ya Afrimma kupitia kipengele cha BEST FRANCOPHONE ambacho kilikuwa kikiwaniwa pia na wasanii kama Fally Ipupa, Toofan, Ya Levis na wenginewe.
Pamoja na halo pia marehemu DJ Arafat alifanya kazi kibao ambazo zilipata umaarufu kama Yorobo, Ventiprontent na hata Touch Body aliyoshirikishwa na J. Martins huku akiwa ameacha sokoni album kumi na moja.