Mfumo wa Android Kuondolewa Kwenye Smartphones

Baada ya miezi kadhaa ya kutoa kauli zinazokinzana sasa wakurugenzi wa kampuni ya bidhaa nyingine za kielektoniki Huawei ya uchina wamefichua mfumo mpya uliotengenezwa na kampuni hiyo kwa ajili ya kuboresha simu za mkononi za Samartphones, vipakatalishi na vifaa vingine vya nyumbani.

Mfumo huo wa Huawei -HarmonyOS unalenga kupunguza utegemezi wake kwa kampuni za Marekani.

HarmonyOS utakuwa tayari kuwekwa katika skrini za samart kwenye bidhaa kama vile Televisheni, saa za smart , na magari baadae mwaka huu, amesema Richard Yu, Mkurugenzi mkuu wa wa kitengo cha walaji cha Huawei katika mkutano wa ubunifu.


Katika kipindi cha miaka mitatu ijayo Huawei,kampuni ambayo ni ya pili kwa ukubwa duniani ya mauzo ya smartphone , itaangalia jinsi ya kuuweka mfumo wa HarmonyOS kwenye vifaa zaidi zikiwemo siku zake za mkononi aina ya smartphones, amesema.

Yu alidai kuwa , bila kutoa ushahidi halisi ,kwamba HarmonyOS ni "yenye nguvu zaidi na bora zaidi ya mfumo Android." "Inaweza kuwekwa katika smartphones? Bila shaka."

" HarmonyOS unaweza kuwekwa katika hali ya kuwa na maingiliano na kifaa kingine chochote kile . Ukitengenezwa kwa njia ya kifaa chenye uwezo wa kusambaza data , HarmonyOS inaweza kujenga mwanzao wa uhusiano shirikishi wa mfumo wa ikolojia," ilieleza taarifa ya kampuni hiyo.

Kampuni ya Huawei inasema kuwa imeazimia kuendelea kutumia Android , lakini HarmonyOS utatumika kama mbango mbadala kama mambo yataenda kombo . "tutaupa kipaumbele mfumo wa Android kwa smartphones, lakini kama hatutatumia Android, tutaweza kuweka mfumo wa HarmonyOS haraka," Yu amesema.

Huawei: 'Marekani hawatuwezi'
Pigo kwa Huawei litakavyoathiri biashara Afrika
Kuwepo kwa mfumo wa simu za mkononi ,ambao ni chanzo cha wazi utakuwa ni kwa ajili ya Uchina pekee kwa sasa, ingawa kampuni ina mipango ya kuuleta katika masoko ya kimataifa baadae , amesema.

Tangazo hilo la Huawei limekuja miezi kadhaa baada ya serikali ya Marekani kuweka masharti ya kibiashara nchini Marekani yanayoilenga kampuni hiyo pamoja na kampuni nyingine washirika .

Serikali ya Marekani imeishutumu Huawei kwa kuiba siri za kibiashara , na ikasema inaleta hatari kwa usalama wa taifa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad