Miili iliyo ungua na Moto Morogoro kufanyiwa DNA


Morogoro. Serikali ya Tanzania imefanya utaambuzi wa vina saba (DNA) kwa miili 21 kati ya 64 iliyotokana na ajali ya moto wa lori lililokuwa limebeba mafuta ya petroli kuanguka na kulipuka eneo la Msamvu mkoani Morogoro.

Sanjari na vifo hivyo, watu 70 waliojeruhiwa, 12 kati yao wamehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam kwa matibabu zaidi huku wengine wakiendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro.

Hayo yalisemwa jana Jumamosi usiku Agosti 10, 2019 na Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu,Sera, Bunge,Ajira, Kazi,Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alipozungumza na wanahabari katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro.

Waziri Mhagama alisema kulikuwa na magari ya kubeba wagonjwa ya kutosha ya kuwachukua majeruhi na kuwawahisha Dar es Salaam.

"Utaratibu wa kuhakikisha majeruhi hao wanasafiri salama barabarani na usalama wao umefanyika chini ya wizara ya mambo ya ndani na vikosi vya usalama barabarani kwa uharaka zaidi."

 "Wizara imetengeneza utaratibu wa kutosha chini ya uangalizi mkubwa kwa timu ya madaktari na wauguzi," alisema
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad