Misri: Gari lilosababisha vifo vya watu 20 lapatikana na bomu



Gari lililosababisha mlipuko katika mji mkuu wa Cairo na kusababisha vifo vya takriban watu 20 na kujeruhi wengine 47 limepatikana likiwa na mabomu ndani.


Polisi walisema kikundi cha Hasm, mshirika mwenye silaha wa Ushirika wa Waislamu,kilikuwa kimetayarisha gari hilo ambalo lilikuwa limeripotiwa kuibiwa miezi kadhaa iliyopita, kutekeleza shambulio la kigaidi.

Mlipuko huo ulitokea nje ya hospitali kuu ya saratani ya Cairo mapema jana na mwendesha mashtaka wa serikali ya Misri ameamuru uchunguzi wa haraka kuhusu tukio hilo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad