Mjane wa Dkt. Reginald Jackline Mengi Atembelewa na Chama Cha Wajane


Chama cha Wajane na Wagane Tanzania (TAWIA), kimemtembelea Mke wa Marehemu Reginald Mengi, Jacqueline Mengi kwa lengo la kumfariji na kumtia moyo.

Akizungumza mara baada ya kupokea ugeni huo, Jacqueline Mengi amewashukuru kwa upendo waliounyesha kwake kwa kipindi hiki kigumu anachopitia.

"Nawashukuru sana kwa upendo nami pia nawapenda, naomba tuendelee kushirikiana kupeana moyo na tuendelee kupendana," amesema Jacqueline.

Amendelea kwa kusema, "Vile vile ningependa kuwapa pole kwa sababu najua haya ninayopitia na nyie mnapitia, naomba niwape pole kwa kufiwa na wake zenu na waume zetu Mungu aendelee kutubariki,"

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad