Mjumbe wa NEC atolewa povu kumlazimisha askari kusalimia kwa salamu ya CCM


Wadau na wanasiasa wamemjia juu Mjumbe wa Halmashauri Kuu Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Pwani Haji Abuu Jumaa baada ya kumlazimisha askari polisi Koplo Said kusalimia kwa salamu ya CCM wakati alipomwagiza kutoa ufafanuzi juu ya masuala ya ulinzi na usalama katika kata ya Vianzi, wilani Mkuranga mkoani Pwani.

Katika video fupi ambayo inatembea mtandaoni mjumbe huyo wa NEC, Pwani anaonekana kumlazimisha askari huyo na pale alipokataa alimwamuru aondoke na maelezo hayo kutolewa na mtendaji wa kata hiyo.

Katika kumlazimisha kwake, Haji Jumaa alitumia mifano ya mabosi wa askari huyo akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ambaye hutembea na ilani ya CCM pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ambaye amewahi kunukuliwa akisalimia kwa kutumia salamu ya CCM.

Askari huyo alikataa na kutoa maelezo kwamba askari hapaswi kuwa na chama chochote cha siasa kwani analinda raia wa vyama vyote.

Kufuatia tukio hilo Maria Sarungi ambaye ni moja ya wanaharakati wa masuala ya haki za binadamu amesema:
“Hivi CCM mnaona sawa kabisa kada wenu kuvunja sheria? Ina maana mpaka leo CCM haielewi miiko ya utumishi wa umma? Enzi ya chama kushika hatamu imekwiisha! Sheria inamkataza polisi kuwa na ushabiki. Wanaofanya hivyo wanakiuka miiko na sheria.”

Naaye Mbunge wa Tarime Vijijini kupitia Chadema John Heche kupitia Twatter yake ameandika: “Tumefika hapa kwasababu wakuu wa jeshi la polisi wametaka iwe hivyo, inakuaje katika karne hii eti kiongozi wa chama fulani cha siasa anaita askari polisi na kumwambia mambo kama haya huyu ni moja walau ameonesha kutotii ujinga, wangapi wanatii mambo mengi ambayo hayaonekani!!



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad